Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sayyid Ebrahim Raisi amesema leo Jumatano katika uwanja wa ndege wa Mehrabad kabla ya kuondoka Tehran akilekea Moscow kwamba: Ziara hiyo inafanyika kwa mwaliko wa Rais Vladimir Putin wa Russia na kwamba juhudi zitafanyika ili kukuza udiplomasia wa kikanda.
Raisi ameongeza kuwa: "Uhusiano mzuri wa Iran na majirani zake wote hususan Russia katika masuala ya kisiasa, kiuchumi na kibiashara, unaweza kuleta mabadiliko makubwa katika uhusiano wetu na Russia."
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Iran ni nchi huru, yenye nguvu na taathira katika eneo la Magharibi mwa Asia, na Russia ni nchi muhimu, yenye nguvu na taathira kubwa.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameondoka mapema leo mjini Tehran akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu.
342/